Angalia shule ulizopangiwa kidato cha tano 2026/2027 kupitia TAMISEMI. Fuata hatua rahisi kuangalia Form Five Selection Tanzania haraka.
Baada ya matokeo ya Kidato cha Nne (CSEE) kutangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), hatua inayofuata kwa wanafunzi waliofaulu ni kupangiwa shule za Kidato cha Tano. Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndiyo yenye jukumu la kupanga wanafunzi katika shule za sekondari za umma na vyuo vya kati kulingana na ufaulu wao na machaguo waliyofanya kupitia mfumo wa Selform. Makala hii inakueleza jinsi ya kuangalia shule uliyopangiwa kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Form Five Selection ni Nini?
Form Five Selection ni mchakato rasmi wa kupanga wanafunzi waliokamilisha Kidato cha Nne kwenda kujiunga na masomo ya Kidato cha Tano (A-Level) au vyuo vya ufundi na diploma. TAMISEMI hushirikiana na NECTA kuhakikisha wanafunzi wanapangiwa kulingana na:
- Ufaulu wao katika mtihani wa CSEE (madaraja na alama / GPA).
- Tahasusi (combinations) walizochagua kupitia mfumo wa Selform, kama vile PCM, PCB, EGM, HGE, HGL, CBG, n.k.
- Nafasi zilizopo katika shule na vyuo husika.
Sifa za Kupangiwa Kidato cha Tano
Ili kupangiwa Kidato cha Tano, mwanafunzi anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe amefaulu mtihani wa Kidato cha Nne kwa kupata Daraja la Kwanza, la Pili au la Tatu (Division I–III). Baadhi ya wanafunzi wa Division III huchaguliwa kulingana na cut-off points.
- Awe na credits tatu (3) au zaidi katika ngazi ya CSEE.
- Masomo yake ya msingi yaendane na tahasusi aliyoiomba.
Shule Walizopangiwa Kidato cha Tano 2026/2027
Serikali kupitia TAMISEMI imetoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2026/2027.
Wanafunzi waliofaulu mtihani wa CSEE wanaweza sasa kuangalia shule walizopangiwa pamoja na combinations zao.
- Form Five Selection 2026 Tanzania
- Shule walizopangiwa kidato cha tano 2026
- TAMISEMI selection 2026
- Jinsi ya kuangalia selection form five
- Majina ya waliochaguliwa kidato cha tano
Jinsi ya Kuangalia Form Five Selection 2026/2027
Fuata hatua hizi rahisi:
👉 Hatua ya 1: Tembelea Tovuti Rasmi
Fungua link hii:
👉 https://selform.tamisemi.go.tz/
👉 Hatua ya 2: Chagua “Selection Results”
- Bonyeza sehemu ya Form Five Selection
- Chagua mwaka 2026
👉 Hatua ya 3: Chagua Mkoa
- Mfano: Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha
👉 Hatua ya 4: Chagua Halmashauri
- Chagua wilaya au council yako
👉 Hatua ya 5: Tafuta Jina Lako
- Angalia jina lako kwenye list
- Utaona:
- Shule uliyopangiwa
- Combination (mfano PCB, EGM, PCM)
Jinsi ya Kuangalia Kupitia Simu
Unaweza kutumia simu yako kwa:
- Browser (Chrome, Opera Mini)
- Kufungua tovuti ya TAMISEMI moja kwa moja
Tip: Tumia internet yenye nguvu ili kuepuka kuchelewa kufunguka kwa site
Vigezo vya Uchaguzi (Selection Criteria)
Uchaguzi wa wanafunzi unazingatia:
- Matokeo ya NECTA
- Performance ya mwanafunzi (division & points)
- Nafasi zilizopo katika shule
- Mchanganyiko wa masomo (combination)
Combination Maarufu Kidato cha Tano
- PCB – Sayansi (udaktari, afya)
- PCM – Uhandisi na teknolojia
- EGM – Biashara na uchumi
- HGL – Arts na social studies
Nifanye Nini Kama Sijachaguliwa?
Kama hujaona jina lako:
- Subiri Second Selection (Awamu ya Pili)
- Angalia nafasi za:
- Vyuo vya kati (Diploma)
- VETA
Kuangalia shule ulizopangiwa kidato cha tano 2026/2027 ni rahisi kupitia mfumo wa TAMISEMI. Hakikisha unafuata hatua zote ili kupata taarifa sahihi kwa haraka.
Soma Zaidi:













Haifunguki password haikibali
Matokeo ya kidato cha tano 2026
MBONA LINK MLIOIWEKA HAIFUNGUKI WAZEE